Upimaji

HATUA ZA AWALI ZA UPIMAJI WA KIWANJA/SHAMBA

 • 1. UKAGUZI WA ENEO NA UTAMBUZI WA MIPAKA.

  1. Wataalamu watafika kukagua eneo na kufanya utambuzi wa mipaka ya eneo husika kwa hatua za awali, Ikiwa ni pamoja na kuchukua taarifa muhimu,
  2. Taarifa hizo zitapelekwa halmashauri husika na wizarani ili kupata usahihi wa taarifa husika ikiwa ni pamoja na mchoro wa mipango miji na kujua eneo hilo limepangiwa matumizi gani kama yalivyo ainishwa kwenye mchoro.

  Gharama za ukaguzi wa eneo husika

  - Mteja atatakiwa kugharamia gharama za ukaguzi wa eneo kama ifuatavyo
  1. Kama atakuwa anamiliki heka moja au kiwanja kimoja, atatakiwa atoe Tsh.200,000/= kama gharama za ukaguzi wa eneo lake au shamba.
  2. Kwa mteja anaemiliki zaidi ya hekari mbili, gharama hizo zitapungua kulingana na idadi ya hekali anazomiliki.
 • 2. MATOKEO YA UKAGUZI WA ENEO HUSIKA

  • A. Eneo linalopimika

   Eneo linalopimika ni eneo ambalo lina mchoro wa mipango miji unaoonyesha matumizi ya eneo husika kama yalivyoainishwa kwenye mchoro husika, kama vile makazi, makazi na biashara, biashara, hoteli,n.k
  • Gharama za upimaji kwenye eneo linalopimika

   Gharama za upimaji kwa Eneo linalopimika hutolewa baada ya UKAGUZI WA ENEO NA UTAMBUZI WA MIPAKA kufanyika, kulingana na mahitaji ya eneo husika, Ikiwa ni pamoja na tathimini ya mpima (surveyor).

   Tathimini hiyo itaonyesha upimaji utachukua mda gani (time frame) na pia inajumuisha ukubwa wa eneo, idadi ya viwanja/hekali, idadi ya mawe (beacons) yatakayopandwa, umbali toka eneo jirani lililopimwa (adjacent survey), gharama za vibarua, gharama za usafiri wakati wa upimaji

  • B. Eneo lisilopimika

   Hii hutokana na eneo husika kutokuwa na mchoro wa mipango miji unaoainisha matumizi halisi.

   Mteja atashauriwa kufanya utaratibu wa kuandaliwa kwa mchoro wa mipango miji kwa eneo husika, ( gharama ya kuandaa mchoro tu 3,000,000 na gharama za kuhakiki mchoro wizarani ni sh 2,000,000) #Ambapo mchoro huo utaandaliwa kwa gharama za mteja

   Baada ya mchoro kupitishwa wizarani eneo husika litakua na hadhi ya kupimika, ambapo hatua za upimaji zitafuata kwa kuzingatia tathmini za eneo husika kama ambavyo zilivyoainishwa katika kipengele 2(a) juu.

   Gharama za kuandaa mchoro wa mipango miji kwa eneo husika zitatolewa kulingana na tathmini halisi za uandaaji wa mchoro kwa halmashauri husika ambapo eneo linapatikana.

   • Hili ni eneo lenye mchoro unaoonyesha matumizi ya umma, tofauti na mahitaji ya mteja, kama vile eneo lililotengwa kwaajiri ya makaburi, maeneo ya wazi (open space), soko, shule,n.k,
   • Mteja atapewa ushauri kulingana na hali halisi ya eneo kama anaweza kufanya mchakato wa kubadili matumizi au lah. Endapo eneo litafaa kubadili matumizi gharama yake itakuwa (4,500,000)
 • 3. KIBALI CHA UPIMAJI

  Mteja au Mmiliki halali wa eneo husika atatakiwa kuandika barua kwa ajili ya kuomba kupimiwa, akiambatanisha hati ya mauziano ya eneo husika na mhutasari wa kikao cha kamati ya ardhi ya mtaa iliyojadili na kupitisha maombi ya kupimiwa. Barua hii itamwezesha Mpima  (surveyor)/ au Afisa mipango miji (Town Planner) kufuatilia kibari cha upimaji katika halmashauri au Manispaa husika, Hii ni kwa yule anayeomba kwa ajili ya upimaji wa kiwanja/ viwanja au kuandaliwa mchoro wa mipango miji

  Kwa anayeomba kupimiwa shamba lake atatakiwa kuandika barua ya kuomba kupimiwa, akiambatanisha hati za mauziano ya shamba hilo yenye mihuli halali kutoka ofisi ya kijiji/kata husika.

 • 4.UPIMAJI

  Mteja ataweza kupimiwa eneo lake baada ya hatua zote kwa mujibu wa sheria za upimaji kufuatwa, ikiwa ni pamoja na vibali kukamilika, Itaandaliwa mchoro (survey plan) na faili (file) ambavyo vitapelekwa wizarani kwa ajili ya ukaguzi na uhakiki wa upimaji uliofanyika kwa kuzingatia taratibu za upimaji,

 • 5. HATI

  Baada ya uhakiki wa michoro na file kufanyika wizarani, file hilo litarudi chini ya usimamizi wa idara ya upimaji na kukabidhiwa kwa mteja husika, tayari kwa yeye (MTEJA) kufuatilia hatimiliki yake.

ANGALIZO: kampuni haitahusika kufuatilia hati ya kiwanja cha mteja, litakua jukumu la mteja kufuatilia hatimliki yake katika halmashauri husika baada ya kukabidhiwa file la upimaji,Kampuni itatoa ushauri na njia bora ya kufuatilia hati kwa mteja pale itakapobidi,