Ujenzi

MKOPO WA VIWANJA, VIFAA VYA UJENZI NA UFUNDI

UTANGULIZI

Mradi utahusika na ujenzi wa nyumba (kuanzia msingi mpaka hatua za mwisho za ujenzi (finishing))

WALENGWA WA HUDUMA

Walengwa wa huduma hii ni watu wote walionunua,wanaonunua viwanja ndani na nje ya kampuni yetu.

HATUA ZA MRADI

 • A. Msingi
 • B. Ujenzi hadi saizi ya madirisha
 • C. Kumalizia hadi linter
 • D. Kuezeka
 • E. Madirisha na milango
 • F. Finishing(kulingana na mteja)

AINA ZA WATEJA

 • A) wateja wanaojenga katika viwanja vyetu tulivyouza-(punguzo asilimia 15 ya gharama za ufundi)
 • B) wateja walionunua yoyote ya huduma na wanajenga sehemu nyingine.(punguzo asilimia 10)
 • C) wateja wanaojenga maeneo yao.

Zingatia:

Gharama za ujenzi zitapungua kwenye gharama za ufundi tu

AINA ZA NYUMBA ZINAZOJENGWA

Aina za nyumba zitatofautiana kulingana na aina ya ramani inayojengwa n.k

GHARAMA NA MFUMO WA KULIPIA

 • Gharama za ujenzi zitatokana na mambo anuwai ikiwemo aina ya nyumba,ukubwa,umbali wa eneo la mradi,upatikanaji malighafi eneo husika.
 • Muda wa kulipia (kila hatua ya ujenzi mteja ataweza kulipia kwa awamu zisizozidi 12,kulingana na uwezo wa mteja
 • Awamu ya kwanza-mteja atalipia asilimia 30% ya gharama za ujenzi wa hatua husika,huku akilipia asilimia 70% ndani ya muda uliobaki pia gharama za ujenzi zitategemea sana na upana wa huduma mfano,kuanzia uandaaji wa Ramani n.k (Ingawa ramani zitatolewa kwa gharama nafuu sana).

TARATIBU ZA KUTOA HUDUMA

 • Mteja atajaza fomu ya maombi husika
 • Timu ya miradi itatembelea eneo husika la mradi.
 • Timu ya miradi itaandaa mchanganuo wa gharama za mradi kulingana na uhitaji wa mteja (ramani,hatua za ujenzi)
 • Pande zote mbili zita saini mkataba,Baada ya makubaliano.
 • Utekelezaji wa mradi utaanza kwa kufuata mkataba.

TIMU YA UTEKELEZAJI WA MRADI

 • Mhandisi(Engineer)
 • Kiongozi wa timu/fundi mkuu(supervisor)
 • Mafundi wasaidizi
 • Wasaidizi

WIWANGO VYA MRADI

M

iradi yote itatekelezwa kwa kufuata viwango halisi vya miradi vilivyokubalika kwenye mkataba.